Joanita:Nipisheni Mkongwe Nimerudi
Mwigizaji aliyewahi kutamba katika sinema za Kibongo, Fatuma Makame ’Joanita’.
Stori: Imelda Mtema
I’AM back! Mwigizaji aliyewahi kutamba katika sinema za Kibongo, Fatuma Makame ’Joanita’ amefunguka kuwa baada ya kupumzika kwa muda katika mambo ya fi lamu, sasa amerejea upya hivyo wale wanaojiita mastaa wakae chonjo.
kizungumza na Ijumaa Wikienda, Joanita ambaye alitamba na sinema kama Sikio la Kufa,Mahaba na Joanita alisema kuwa alipumzika kwa ajili ya malezi baada ya kujifungua lakini sasa amerudisha nguvu zote kwenye kazi yake na yuko mbioni kuachia kazi zake mpya.
“Mkongwe nimerudi kazini, wanajiita mastaa wa fi lamu wanipishe maana nina ari mpya kabisa na ninajua wapenzi wangu watakuwa wana hamu ya kupata ladha tofauti,” alisema Joanita.

