Job Ndugai apitishwa na CCM kuwania Uspika
Job Ndugai.
MBUNGE wa Kongwa na aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoisha, Job Ndugai amepitishwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (ccm) kugombea nafasi ya Uspika baada ya wagombea wengine wawili waliopitishwa mwanzo kujitoa.
Wagombea waliojitoa ni pamoja na Ndugu Abdullah Ali Mwinyi na Dk. Tulia Ackson Mwansasu.