Jogoo Afikishwa Mahakamani kwa Kosa Hili, Ajizolea Umaarufu!

JOGOO mmoja ambaye mmiliki wake amempatia jina la Maurice, amekuwa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri na hivyo kufikishwa katika mahakama moja nchini Ufaransa.

 

Maurice analalamikiwa kwa kusababisha kelele kwa familia moja katika Kisiwa cha Oléron huko Ufaransa ambapo mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote hufanya —  ‘kuwika’.

Waliomshtaki Maurice na Maurice mwenyewe hawakufika mbele ya mahakama ya mji wa Magharibi wa Rochefort siku ya Alhamisi kesi ilipoanza kusikilizwa,  lakini jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama.

 

Walalamikaji ambao ni Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, wamesema walijenga nyumba yao ya mapumziko katika kijiji cha Saint-Pierre-d’Oléron karibu miaka 15 iliyopita, lakini baadaye wakaigeuza kuwa nyumba ya kuishi walipostaafu.

Sababu moja iliyowafanya kuchagua sehemu hiyo ni utulivu wake lakini tatizo ni kuwa jogoo Maurice; amekuwa kero kwao kwani amekuwa akiwapigia kelele kila alfajiri anapowika. Wanasema tatizo hilo lilianza tangu mwaka 2017 jirani yao alipomnunua.

 

Walipowasilisha lawama zao kwa Bi Fesseau, ambaye ameishi Oléron kwa miaka 35, mabishano makali yalizuka mpaka mzozo kati yao ukagonga vichwa vya habari ulipofikishwa mahakamani.

Bi. Fesseau, na majirani zake wengine, walisema hakuna mjadala kuhusu jambo hilo kwa sababu ufugaji wa kuku ni sehemu ya maisha ya vijijini na kwamba hawaelewi kwa nini walalamishi wanaomba jogoo huyo azuiwe kuwika.

 

Utatuzi wa mzozo huo unasalia na mahakama ambayo inasubiriwa kutoa uamuzi wa kesi mwezi Septemba mwaka huu.

INASIKITISHA! Askari AJINYONGA Kisa MAMA Mkwe, MASHUHUDA Wasimulia!

 


Loading...

Toa comment