The House of Favourite Newspapers

Joh Makini Amtamani Fid Q

Joh Makini

Rapa anayekimbiza gemu la Muziki wa HipHop Bongo, Joh Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’ amesema ipo siku atamshirikisha Fid Q katika ngoma yake maana ni msanii mzuri ambaye anatamani kufanya naye kazi.

Fid Q

Akistorisha na Gazeti la Amani, siku moja baada ya Fid Q ‘kushow love’ kwa kusapoti kazi za Joh kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram jambo lililoibua gumzo kutokana na kuhusishwa kwenye bifu, Joh amesema yeye na Fid wapo freshi na hawajafanya kazi pamoja kwa sababu bado hakujatokea ‘chemistry’ ya kuwakutanisha.

“Siku nikiwa na vibe ya kufanya ngoma na Fid nitafanya naye, ninamtamani kwa sababu ni msanii mzuri na ninashukuru kwa sapoti yake,” alisema Joh.

Save

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Save

Comments are closed.