The House of Favourite Newspapers

Joh Makini Kuachia Ngoma na Davido Soon

Davido na Joh Makini wakiwa na wacheza shoo wao katika maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo.

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Joh Makini, yupo mbioni kuitimiza ahadi aliyowaahidi mashabiki wa muziki huo nchini. Joh Makini aliahidi kufanya wimbo mmoja atakaoshirikiana na staa kutoka Nigeria, Davido.

Mapema leo kwenye mitandao ya kijamii imekuwa ikisambaa picha ambayo inawaonyesha wasanii hao wakiwa katika matayarisho ya video ya wimbo huo.

Aidha Joh Makini bado hafunguka kwa mashabiki wake jina la wimbo huo na kwa upande wa Davido jamaa ametupia picha katika mitandao ya kijamii na kuandika ujumbe  “Back to Work On Set Shoot @Johmakini Feat Davido. Aliandika Davido.

 

Comments are closed.