Johari Abariki Ndoa ya Ray na Chuchu

MKONGWE wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa hakuna kitu kitakachomfurahisha kama mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ akimuoa mzazi mwenziye, Chuchu Hans.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend, Johari aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Ray alisema kuwa, anatamani hivyo kwa kujua wazi kabisa kuwa Chuchu ni sahihi la Ray maana ni mwanamke ambaye amemzalia mtoto mzuri.

“Kiukweli nitafurahi sana mkurugenzi mwenzangu (RJ Company) akimuoa Chuchu. Kwanza ni mwanamke wa chaguo lake na pia amemzalia kidume cha nguvu na kwenye harusi nitakuwa mstari wa mbele,” alisema Johari.

Na Imelda Mtema

Loading...

Toa comment