The House of Favourite Newspapers

JOHARI AFANYA MAOMBI MAALUM KUONDOA MIKOSI

Image result for Blandina Chagula ‘Johari
Blandina Chagula ‘Johari’

MREMBO mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema mwezi Septemba ulikuwa mbaya kwake kutokana na kuandamwa na matatizo hivyo mwezi huu amefanya maombi maalum ili kujiondolea mikosi.

Johari alisema mwezi uliopita aliibiwa, alipata ajali ya gari hivyo kwake anaona si kawaida kwa hiyo anamuomba Mungu amuepushe na mabalaa ili aweze kumaliza mwaka vizuri.

 

“Ulikuwa mwezi mgumu kwangu, nimepitia kwenye changamoto za mfululizo lakini namshukuru Mungu nipo imara. Nafanya maombi maalum Mungu aniepushe na mabalaa,” alisema Johari ambaye ni mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ anayoshirikiana na muigizaji
mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Stori: Mwandishi Wetu

Comments are closed.