The House of Favourite Newspapers

Johari afunga mwaka kwa maombi

johari1

Na Hamida Hassan, Gazeti la Ijumaa, Toleo la Desemba 30, 3016

Staa wa Filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameufunga Mwaka 2016 kwa maombi ambayo alifanyiwa na watoto yatima wa Kituo cha Sifa Foundation.

Zoezi hilo alilifanya hivi karibuni kwenye kituo hicho kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo mwenyewe alieleza kuwa, amefanya hivyo ili kujiondolea balaa na Mwaka wa 2017 uwe ni wa mafanikio kwake.

“Kiimani watoto wakikuombea dua, inakwenda kwa Mungu moja kwa moja. Nimekuwa na amani sana baada ya kufanyiwa maombi hayo na naamini yale ninayoyapanga kwa Mwaka 2017 yatafanikiwa,” alisema Johari.

Comments are closed.