The House of Favourite Newspapers

Johari Kumwanika Mrithi Wa Ray

 

johari1

Mwigizaji Blandina Chagula ‘Johari’.

Stori: Mwandishi Wetu

KUFUATIA kuwepo kwa kiu ya mashabiki wake kutaka kumjua mpenzi wake kwa sasa anayetembea naye baada ya kumwagana na Vincent Kigosi ‘Ray’, mwigizaji Blandina Chagula ‘Johari’ amewataka mashabiki wake wasiwe na wasi, watamjua mhusika.

RAY2334Staa wa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Johari alifunguka hayo hivi karibuni maeneo ya Ubungo jijini Dar baada ya paparazi wetu kumkuta nje ya baa moja akiwa na njemba mmoja hivi wakila raha zao na alipoulizwa kama huyo ndiye shemeji kwa sasa, Johari alikataa na kusema watu wasubiri watamjua tu.

“Siyo huyu bwana, nilijua tu utauliza hilo swali. Huyu ni mshkaji wangu tu anaitwa Freedom nimefanya naye muvi inaitwa Dosari na huwa ananipa kampani sehemu tofautitofauti,” alisema Johari.

Comments are closed.