The House of Favourite Newspapers

Johari: Sina Muda na Ray Kwa Sasa Nipo Bize na Kampuni Yangu ya Lokoma

0
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula almaarufu Johari.
Blandina Chagula almaarufu Johari ; ni muigizaji wa sinema za Kibongo ambaye anasema kuwa, hana muda wa kumfikiria aliyekuwa patna wake, Vincent Kigosi au Ray  kwani yupo bize na kampuni yake mpya.

Johari anasema kuwa, yeye na Ray ni zilipendwa na sasa anapambana na maisha yake kwa kushirikiana na mbia wake Chifu ambaye ni Mkurugenzi mwenza katika kampuni yao ya Empire Lokoma.
Vincent Kigosi au Ray.

“Tunazalisha tamthiliya, sasa hivi niko bize na Tamthilia ya Maji ya Shingo inayoruka Azam TV, kuna kazi nyingine nzuri zinakuja hivyo watu wangu wakae mkao wa kula,” anasema Johari.

Johari alikuwa mbia kwenye Kampuni ya RJ na Ray, lakini ilifika wakati wakaachana na sasa kila Mtu anapiga mzigo kivyake.

Leave A Reply