Kartra

John Bocco Asepa Na Tuzo Ya Mchezaji Bora

JOHN Bocco kinara wa mabao ndani ya ardhi ya Bongo amechaguliwa kuwa mchezaji bora kwa mwezi Juni.

Bocco ametupia mabao 15 anafuatiwa na Prince Dube mwenye mabao 14 ila anakipiga Azam FC.

Ndani ya mwezi Juni, Bocco alitupia mabao matatu baada ya Simba kucheza mechi tatu na ilishinda mechi zote hizo na kubaki nafasi ya kwanza.

Aliwashinda wachezaji wenzake wawili ambao aliingia nao fainali ambao ni Feisal Salum wa Yanga pamoja na Idd Seleman wa Azam FC.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa leo Julai 16 na Bodi ya Ligi Tanzania.


Toa comment