The House of Favourite Newspapers

John Bocco: Azam anakufa leo

WAKATI leo Jumatano Simba ikitarajiwa kuwa wenyeji wa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, straika wa timu ya Simba, John Bocco amefunguka kuwa kwenye mchezo huu wanashuka dimbani wakiwa na lengo moja la kupata matokeo mazuri.

 

Mshambuliaji huyo mwenye mabao tisa kwenye ligi, ataiongoza timu yake hiyo ya Simba kucheza na Azam ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwenye mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, straika huyo alisema: “Hakuna cha kupoteza kwenye mchezo huu, tunataka tushinde kwa ajili ya kuendeleza rekodi yetu iliyopita kwenye mechi tano ambazo zote tuliibuka na ushindi.

 

“Tunajua wapinzani wetu ni wazuri na wenye timu yenye ushindani lakini kwetu hatutaangalia hilo, kikubwa tunajipanga kupata matokeo mazuri mbele yao na wote kwa pamoja tunaamini tutalikamilisha hilo kwa umoja wetu,” alisema.

 

Hadi sasa Simba ndiyo vinara wa ligi wakiwa na pointi 38 baada ya mechi 16 za ligi kuu wakifuatiwa na Azam ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 33.

 

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.