The House of Favourite Newspapers

John Kerry Atembelea Eneo Ambapo Alimuua Hasimu Vitani

0

   john-terry4 John Kerry akindamana na mwanahistoria Edward Miller

Vietnam: Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni wa Marekani anayemaliza muda wake, John Kerry, amezuru eneo moja nchini Vietnam, ambapo alivamiwa wakati wa Vita vya Vietnam.

Kerry ambaye ni mwanajeshi mwanamaji wa zamani wa Marekani alikutana na mpiganaji wa zamani wa Vietnam, Bwana Tam mwenye umri wa miaka 70 ambaye anakumbuka shambulizi hilo la mwaka 1969 ambapo wawili hao walisalimiana kwa kupeana mikono

john-terry3 John Kerry akitumia ramani kutambua eneo ambapo shambulizi lilitokea

Kerry alimuambia hasimu wake huyo wa zamani Vo Ban Tam, kuwa ni vizuri wote wako hai. Bwana Tam ambaye sasa ni mkulima, anasena anafahamu mtu ambaye Kerry alimuua na pia anakumbuka njama yao ya kushambulia mashua ya Marekani.

john-terry2

John Kerry (kushoto) akizungumza na mpiganaji wa Vietnam, Vo Ban Tam (wa pili kulia)

Bwana Kerry ambaye yuko nchini Vietnam kwa ziara yake ya mwisho kabla ya kuondoka madarakani, alitunukiwa kwa ujasiri wake vitani enzi hizo. john-terry1

John Kerry akiwa eneo ambapo alipigana vita vya Vietnam

Kerry ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 26, alitunukiwa kwa kukinusuru kikosi chake baada ya kumpiga risasi na kumuua mtu ambaye alikuwa akipanga kushambulia mashua yao kwa kombora.

Leave A Reply