John Mnyika: Barua ya Baraza Kuu ya Kutupilia Mbali Rufaa za Wakina Mdee Imeshafika kwa Spika
Mnyika ameandika ujumbe huo baada ya Leo Mei 13, 2022 baadhi ya wabunge hao kuonekana bungeni kama ilivyokuwa awali kabla ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la CHADEMA kutupilia mbali rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Kamati Kuu kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
“Barua kuhusu Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama 19 CHADEMA imeshafika kwa Spika. Hii ni barua ya pili baada ya ile ya kufukuzwa kwao uanachama na Kamati Kuu mwaka 2020. Spika ni vyema akaheshimu na kutekeleza sasa matakwa ya katiba ya nchi na sheria,” John Mnyika.