John Legend Ajikita katika Biashara Ya Bangi

MWANAMUZIKI Mmarekani, John Legend,  ameungana na kampuni moja nchini Marekani kama mwekezaji kwenye biashara ya bangi ambayo itazinduliwa rasmi Jumanne ijayo.

 

“Nimekuwa muumini katika faida za bangi kwa muda mrefu,” alisema Legend kwenye taarifa yake na kuongeza:  “Nilivutiwa kufanya kazi na timu hii kwa sababu wao ni kampuni ya ubunifu, inayoendeshwa na familia, na hutumia sayansi kutoa bidhaa thabiti, yenye ubora wa juu. Ninashukuru kuwa wamejitolea kuweka viwango vya hali ya juu ndani ya tasnia ambayo hadi leo haijazingatiwa. ”

 

Bidhaa hizo ambazo zitaingia sokoni kwa dola 35 za Marekani, zitapatikana kwenye ladha za zabibu, hudhurungi na chai ya kijani.

“Kuupa ulimwengu njia rahisi ya kufikia usawa imekuwa dhamira yetu kila wakati, biashra yetu inaturuhusu sisi kupanua wigo kutoka California hadi majimbo karibu yote hamsini. Tunafurahi kwamba John Legend ameungana na timu yetu kuunga mkono mpango huu mpya wa kusisimua, “alisema Jake Heimark, Mkurugenzi Mtendaji na mmoja wa waanzilishi wa biashara hiyo.

Legend ameingia kwenye orodha ya mastaa wa muziki wanaofanya biashara ya bangi wakiwemo Post Malone, Wiz Khalifa na Jay-Z ambaye mwezi Julai alitangaza kuungana na kampuni moja iliyopo San Jose kama mtaalam mkuu wa bidhaa.


Loading...

Toa comment