The House of Favourite Newspapers

Johnny Depp Amuangukia Trump

0

Ikiwa Saa chache baada ya kusimama jukwaani na kutoa maneno ya utani kwamba angeweza kumuua Rais Donald Trump, muigizaji mwenye jina kubwa Hollywood, Johnny Depp ameibuka na kumuomba msamaha rais huyo kama ishara ya kumpigia magoti.

Ikumbukwe kuwa muigizaji huyo alisimama katika sherehe za Glastonbury na kuuliza ni lini ilikuwa mara ya mwisho kwa muigizaji kumuua rais wa Marekani kitu ambacho kilitafsiriwa kwamba hata yeye alikuwa na uwezo wa kumuua rais huyo.

“Ni utani mbaya! Sikuwa na maana kwamba nilitaka kumuua. Naomba anisamehe kwa utani wangu,” alisema Depp.

Leave A Reply