Jokate atoa ya moyoni followers mil. 5

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwigelo amefurahishwa na idadi ya wafuasi kwenye ukurasa wake wa Instagram kuongezeka hadi kufikia milioni 5.  Akizungumza na Amani, Jokate alisema amekoshwa sana na wananchi kumkubali kiasi hicho ambapo anawaahidi kuwatumikia kwa moyo wake wote kwenye eneo lake pamoja na Watanzania kwa ujumla.

“Ukweli nimefurahishwa sana na wananchi, kufikisha watu milioni 5 sio mchezo jamani, nawaomba wazidi kuni-support kwani ndoto yangu ni kutumikia wananchi kwa moyo na uwezo wangu wote,” alisema Jokate


Loading...

Toa comment