The House of Favourite Newspapers

Jokate: Nimemchoka Kiba!

0

IMG-20151118-WA0010Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.

STORI: Waandishi Wetu

Yamekuwa yakitokea mambo mengi kwenye uhusiano wa mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Salehe Kiba ‘Ali Kiba’, mara wamwagane, mara wazichape lakini safari hii inaonekana mwisho umefika, Ijumaa lina kitu exclusive.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa, Jokate amefunguka laivu kumchoka jamaa yake huyo akidai si mwanaume anayeweza kumfikisha pale anapopataka.

Tujiunge na chanzo
Hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake alieleza kuwa, uhusiano wa Kiba na Jokate umefika tamati kufuatia malalamiko ambayo Jokate amekuwa akiyatoa akidai, staa huyo wa kibao cha Nagharamia amekuwa haeleweki, hali inayosababisha mambo yao kutowaendea vizuri.

aliiiiilMwanamuziki Ali Salehe Kiba ‘Ali Kiba.

“Yaani nyie hamjui tu lakini ukweli ni kwamba Jokate kamchoka Kiba kutokana na mambo yake na ameamua sasa kuchukua hamsini zake, mwenyewe anasema amekuwa akimshauri mambo mengi kuhusu maisha yao tena ya kimaendeleo lakini Kiba amekuwa akiyapotezea.

“Jokate anasema, yeye ni mwanamke mpambanaji hivyo anapokuwa na mwanaume, lazima awe anayeshaurika lakini kwa Kiba imekuwa ni tofauti. Akishauriwa hili, linaingilia huku na kutokea huku.
“Ukichanganya na haya madai yule Sabby kuwa kuna sms zimenaswa akichati na Kiba ndiyo kabisaa shosti wangu kachoka na kaamua kuwa na maisha yake,” alisema mtoa habari huyo.

Ni yaleyale ya kwa Diamond
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, Jokate anaona kama aliyokuwa akiyaona kwa Diamond kipindi kile ndiyo anayokumbana nayo sasa, hivyo anajitafakari upya aina ya wanaume wa kuwa nao kwenye uhusiano.

kiba-na-jokatee (1)…Wakiwa kwenye pozi la mahaba.

“Yaani yeye anachosema ni kwamba, haoni tofauti ya hawa wanaume wawili, Kiba na Diamond na anavyoonekana si mtu wa kuja kuwa na mpenzi ambaye ni mwanamuziki,” kilifunguka chanzo hicho.

JOKATE ANASEMAJE?
Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa lilifanya jitihada za kuzungumza na Jokate mwenyewe ambapo alipopatikana alifunguka kwa kifupi: “Hayo mambo na Ali (Ali Kiba) yamenichosha, sasa nyie hicho mlichoambiwa andikeni lakini mimi siwezi kuongea.Ijumaa: Angalau ufunguke kidogo sababu hasa za kumchoka mshkaji ukiacha hizo ambazo tumeambiwa na chanzo.
Jokate: Sina la kusema.

Ijumaa: Au imekuuma kusikia anatoka na yule Sabby Angel? Funguka mama.
Jokate: Kama huyo Kiba anampenda sana huyo Sabby naamchukue kabisa, mimi nina maisha yangu sasa, halafu naomba mniache jamani!

Kiba kama kawa
Baada ya kumsikia Jokate a.k.a Kidoti, Ijumaa lilimvutia waya Kiba lakini kama kawaida yake simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Jitahida za kumpata bado zinaendelea.

Leave A Reply