Jokate noma, alishika namba 2 Miss Tz, lakini…!

LINAPOTAJWA jina la Jokate Mwegelo, kila mtu ana namna anavyomjua. Wengine watakwambia kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, basi alikuwa mshindi wa pili wa Miss Tanzania mwaka 2006/07.

 

Wengine watakuambia alikuwa mwigizaji mzuri wa Bongo Muvi aliyetwaa tuzo kadhaa. Wapo watakaokuambia alikuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva. Wengine watakwambia wanamjua kama mtangazaji wa Channel O.

 

Wapo wanaomjua kama mwanamitindo na mshereheshaji (MC). Pia mkurugenzi wa Kampuni ya Kidoti ambayo hujihusisha na ubunifu wa mavazi na kuwavalisha watu.

 

Pia wapo wanaomjua Jokate kama mhamasishaji na amekuwa mfano wa kuigwa kiasi cha kumfanya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ amuone na kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na huko anaendelea kuweka rekodi zake. Vyeo vyote hivyo Jokate amevipata kutokana na Miss Tanzania 2006/07. Wapo wengi waliotwaa taji hilo, lakini hawamfikii Jokate hata robo kwa mambo aliyoyafanya.

MAKALA: SIFAEL PAUL, DAR

List yaMastaa Wa Bongo Wanaoishi Kwenye Nyumba Za Ghorofa

Toa comment