The House of Favourite Newspapers

Mkude Anusurika Ajali ya Gari Akitoka Dodoma

0
Gari lenye namba za usajili T 834 BLZ, Toyota VX alilokuwa akisafiria nahodha wa timu ya Simba, Jonas Mkude, na wenzake ambao hawakufahamika mara moja, likiwa limepinduka na kuanguka vichakani katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam.

Kiungo na nahodha wa timu ya Simba SC, Jonas Mkude amepata ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria na abiria wengine kupinduka katika eneo la Dumila mkoani Morogoro wakati wakirejea jijini Dar es salaam kutokea Dodoma.

Thomas Mkude.

Ajali hiyo iliyohusisha  gari yenye namba za usajili T 834 BLZ, Toyota VX imetokea baada ya gurudumu la nyuma ya gari hiyo kupasuka na kusababisha majeruhi wawili ambapo wamewahishwa kwenye hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Leave A Reply