Jordin Sparks amtema mpenzi wake

jordin-sparks-ai-season-finale-18Jordin Sparks.

NEW YORK, Marekani
YUPO sokoni? Staa aliyetolewa na shindano la kuibua vipaji la American Idol, Jordin Sparks anadaiwa kumtema mpenzi wake ambaye naye ni msanii, Sage The Gemini baada ya kuwa naye kwa miezi 10.

Mrembo huyo ambaye alitisha sana kupitia Kibao cha No Air, kabla ya kuwa na rapa Sage The Gemini alikuwa akitoka na Jason Derulo kisha akatemana naye mwaka juzi.

ouiouiououououoJordin Sparks akiwa na Sage The Gemini.

Hivi sasa ukiingia kwenye akaunti ya Instagram ya mwanadashosti Jordin hakuna picha yoyote ya Sage The Gemini tofauti na awali ambapo alikuwa akijaza ‘selfie’ zao hali iliyoibua maswali kibao kuhusu uhusiano wa wawili hao kama yaliyomo yamo.Lakini mpaka sasa hakuna mmoja wao aliyejitokeza kuzungumzia ‘rumaz’ hizo.

Loading...

Toa comment