The House of Favourite Newspapers

Joshua Achaguliwa Kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa

0
Aliyechaguliwa kuwa Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya sengerema, Joshua Shimiyu  kuwa wajumbe wa mkutano mkuu Taifa CCM.
Aliyewahi kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Sengerema kupita CCM Joshua Shimiyu nimiongoni mwa wajumbe watatu waliochaguliwa na mkutano mkuu wa CCM wilaya ya sengerema  kuwa wajumbe wa mkutano mkuu Taifa CCM.
Wengine waliochaguwa ni Dr Omari Sukari na Jackrini George waliopata kura kwa wajumbe wa mkutano huo,
Joshua akizungumuza na waandishi wa habaru  mara baada ya kuchaguliwa amewashukuru wanaCCM kwa kumpatia heshima hiyo  amewataka wanaCCM kupokea zawadi ya utushimishi na uwakilishi uliotukuka.
” Ninawashukuru wanaCCM mumenipa heshima kubwa nitawatumikia kwa moyo mmoja ” amesema Joshua.
Baadhi ya wajumbe wa  Mkutano huo wamesema kuchaguliwa viongozi hawa ambao watakuwa wawakilishi bora  ngazi ya Taifa.
Katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Muhusin Zikatumu amesema wanaCCM wametumia haki yao kikatiba kwa kuwapata viongozi wanaowataka.
Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza kimekamilisha uchaguzi wake ngazi ya wilaya ambapo Marco Makoye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema kwa kupata kura 1178, huku uchaguzi wa katibu mwenezi ukiahilishwa.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa uliochaguliwa wametakiwa kuwatumikia wananchi ili wapige hatua kimaendeleo
Leave A Reply