The House of Favourite Newspapers

JOSHUA AMCHAKAZA KWA TKO POVETKIN RAUNDI YA SABA (Picha+Video)

Mwingereza Anthony Joshua akiwa na mataji yake manne ya IBF, WBA, WBO na IBO baada ya kumtwanga Povetkin raia wa Urusi.

MWINGEREZA Anthony Joshua amevunja rekodi ya bondia Povetkin,  raia wa Urusi, kwa kumpiga kwa ‘Technical Knock Out’ round ya saba ya pambano kati yao kwenye Uwanja wa Wembley usiku wa kuamkia leo.

Povetkin (kulia) akiwa chini baada ya kupigwa raundi ya saba.


Kabla ya bondia Alexander Povektin kupoteza pambano hilo dhidi ya Anthony Joshua kwa TKO, hilo  linakuwa pambano lake la pili kupoteza katika mapambano 36 aliyocheza akishinda 34, KO 24 huku Joshua akiendelea na rekodi ya kutopigwa.

Anthony Joshua akimtwanga Povetkin.

Kabla ya pambano hilo Joshua alikuwa akishikilia mataji matatu kati ya manne makuu ulimwenguni katika uzito wa juu (IBF, WBA na WBO) na baada ya ushindi ameongeza taji la IBO World.

JEFF POWELL’S SCORECARD
JOSHUA ROUND POVETKIN
9 1 10
10 2 9
9 3 10
10 4 9
9 5 10
9 6 10
56 TOTAL 5

Comments are closed.