The House of Favourite Newspapers

Joti, Mc Regan Nusura ‘Waue’ Tabora

0

Wasanii wa Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhuvile ‘Joti’ na mwenzake Alex Chalamila ‘McRegan’.

Na Richard Bukos, Tabora

Wasanii wa Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhuvile ‘Joti’ na mwenzake Alex Chalamila ‘McRegan’ hivi karibuni walizua tafrani ya aina yake na kutaka kusababisha vifo baada ya kupanda kwenye jukwaa la kampeni za CCM zilizofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Tukio hilo lilitokea baada ya umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo kwa ajili ya kusikiliza kampeni za mgombea urais, John Magufuli kila mmoja kutaka kusogea mbele ili kuwaona wasanii hao wakitoa burudani, hali iliyosabisha watu kukanyagana na wengine kuangushwa chini.

Hata hivyo, watu wa usalama waliokuwa eneo hilo walifanya kazi ya ziada kuhakikisha hali inakuwa shwari.Katika kampeni hizo, licha ya burudani kibao mgombea urais aliwaacha midomo wazi wananchi baada ya kutumia lugha zaidi ya ishirini kwa ufasaha katika kuomba kura.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply