Jovago kutoa ofa ya Valentine kwa wapendanao

JOVAGO (3)

Mkurugenzi Mtendaji wa Jovago Afrika Mashariki, Estelle Verdier-Watine (aliyesimama) akiongea na wanahabari kuhusu faida za kutumia mitandao ya kijamii.

JOVAGO (2)

Meneja Uhusiano wa Jovago Tanzania, Lilian Kisasa akielezea kwa wanahabari jinsi Jovago na Hoteli ya Ramada walivyojipanga kutoa zawadi kwa wapendanao Siku ya Valentine.

JOVAGO (1)

Meneja wa Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni akieleza faida za mitandao ya kijamii katika kukuza sekta ya utalii nchini.

KAMPUNI ya Jovago ambayo huwawezesha wateja kufanya booking katika hoteli mbalimbali kwa njia ya mtandao ndani na nje na nchi imeandaa shindano litakalowawezesha wapendanao kupata ofa ya kulala katika hoteli ya kisasa ya Ramada Siku ya Wapendano (Valentine’s Day), Februari 14 mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari jana katika Ofisi za Jovago Tanzania zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Jovago Tanzania, Lilian Kisasa alisema kampuni hiyo imeandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Hoteli ya Ramada ya jijini Dar es Salaam na mshindi ni yule atakayefanikiwa kupata idadi nyingi ya ‘LIKE’ mara baada ya ku-post kwenye ukurasa wake wa Instagram picha itakayokuwa imewekwa kwenye ukurasa wa Jovago-Instagram na kisha kuweka ‘hash-tag’ ya neno #JOVAGOVALENTINE.

Lilian aliongeza kuwa mshindi pamoja na mwenza wake watapata ofa ya kulala katika hoteli hiyo ya kisasa na kulipiwa gharama za chakula kwa usiku mmoja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jovago Afrika Mashariki, Estelle Verdier-Watine wakati akiongea na wanahabari alisema huu ni muda muafaka kwa Watanzania kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kutengeneza fedha na kukuza uchumi wa taifa hasa kupitia utalii.

Aliongeza kuwa Jovago imeamua kutoa ofa hii ili kuhamasisha utalii nchini na kueleza kuwa mitandao ya kijamii ikitumika vizuri inaweza kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwa urahisi na gharama nafuu.


Loading...

Toa comment