The House of Favourite Newspapers

Jovago kuwafikia watu wa kima cha chini

0

jovago-1

Mkurugenzi Mkuu wa Jovago, Paul Midy akiongea na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Meneja wa Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni.

jovago-2

Mkurugenzi Mkuu wa Jovago, Paul Midy akielezea faida za Jovago kwa wanahabari. Kulia aliyesimama ni Meneja wa Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni.

jovago-3

Paul Midy akifafanua jambo kwa mwanahabari wa BBC. Kulia ni Andrea Guzzoni na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Jovago, Lilian Kisasa.

jovago-4

Viongozi hao wakimsikiliza kwa makini mwandishi wa BBC.

Na Clarence Mulisa

KAMPUNI ya Jovago inayojishughulisha na kuweka oda ya huduma za mahoteli mbalimbali kwa njia ya mtandao ndani na nje na nchi imejipanga kuwafikia watumiaji wa kima cha chini kwa haraka.

Akizungumza na wanahabari leo katika Ofisi za Jovago Tanzania zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Jovago, Paul Midy, amesema Jovago imejipanga kuhakikisha inawafikia wateja wote wakiwemo wa kima cha chini katika utoaji huduma za mahoteli.

Midy amesema kwa sasa tayari wameingia makubaliano na mahoteli mbalimbali yakiwemo ya bei za chini yaliyopo sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi na kuyataka mahoteli ambayo yanataka kuingia nao makubaliano kutosita kuwasiliana nao ili waunganishwe na Jovago.

“Jovago tumekuja kuondoa changamoto ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikiwakabili wananchi ikiwemo dhana kwamba mahoteli siku zote ni gharama na kushindwa kuchagua hoteli za bei za chini lakini kwa kupitia Jovago mteja ataweza kuchagua hoteli aitakayo na bei ambayo ataimudu huku akitumia njia mbalimbali za malipo ikiwemo mitandao ya simu kama Tigo Pesa na M Pesa.

Milango ipo wazi kwa wenye hoteli kuja na kufanya makubaliano na sisi ili tuweze kufanya nao kazi na kuzifanya hoteli zao ziweze kupata wateja kutoka sehemu mbalimbali za dunia.”

Naye Meneja wa Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni amesema watumiaji wa Jovago hivi karibuni wataweza kutembelea tovuti yao ya www.jovago.com kwa kutumia lugha ya Kiswahili ambayo itarahisisha huduma kwa wateja hasa wanaotumia lugha hiyo katika kuweka oda zao za mahoteli.

Jovago.com ambayo ni tovuti namba 1 kwa kutoa oda ya huduma ya mahoteli barani Afrika, ilianzishwa mwaka 2013 na kwa sasa tayari ina zaidi ya hoteli 25,000 inayofanya nazo kazi katika zaidi ya nchi 40 za Afrika huku ikiwa na hoteli zaidi ya 200,000 duniani kote.

Kwa watumiaji wa simu za mkononi, wanaweza kupata huduma za Jovago kwa kupakua ‘App’ ya Jovago kupitia ‘Google Play’ bure na kufurahia huduma za kuweka oda ya hoteli wazitakazo popote duniani.

 

 

Leave A Reply