JPM Aagiza Askari Mwanamke Apandishwe Cheo

RAIS John Magufuli ameagiza polisi wa kike, WP 4160 Beatrice Kayuni Mlanzi, kupandishwa cheo kutoka Koplo na kuwa Sajenti baada ya kuonyesha utimilifu katika kazi. Agizo hilo amelitoa jana Septemba 10, 2019, baada ya kupita katika kituo cha Polisi Selander Bridge.

 

Magufuli alipita kituoni hapo akiwa njiani kurejea Ikulu, akitokea Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokwenda kumjulia hali Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Rais alikwenda kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa.


Loading...

Toa comment