JPM Aanika Mchezo Polisi Walivyokula Mil 700 Kusindikiza Dhahabu ya Magendo -Video

Rais Magufuli akimuapisha Doto Biteko kuwa Waziri wa Madini. Kabla ya Uapisho huo, Biteko alikuwa Naibu Waziri wa Madini. Hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Januari 9, 2019.

 

RAIS John Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa kushughulikia suala la dhahabu ya magendo iliyokamatwa mkoani Mwanza, Januari 4, mwaka huu, ambapo polisi wanaodaiwa kuindikiza dhahabu hiyo walitiwa mbaroni na wengine kuvuliwa vyeo.

 

Magufuli amesema hayo leo Jumatano, Januari 9, 2019 baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana akiwemo Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

 

Rais Magufuli akimuapisha Bi. Dorothy Mwaluko kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji). Kabla ya Uapisho huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 

 

“Nakupongeza sana IGP kwa kushughulikia suala la madini kule Mwanza, umefanya vyema kuwakamata wale askari waliokuwa wakizungumza na mtuhumiwa ili wapewe rushwa. Walishapewa Sh. Milioni 700 na nyingine waliambiwa watapewa Sengerema.

 

“Kwa taarifa nilizonazo, watuhumiwa wale walishikwa Januari 4, wilayani Misungwi, wakarudishwa mjini Mwanza na kikosi cha polisi annane, wakawapeleka Central wala hawakuwaingiza ndani.  Watuhumiwa walikuwa kwenye gari, wakawa wanajadili namna ya kuwapa hela, wakawaambia watawapa bilioni moja na usiku wakaondoka.

Rais Magufuli akimuapisha Arch. Elius Mwakalinga kuwa Katibu Mkuu Ujenzi. Kabla ya uapisho huo Arch. Mwakalinga alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na anachukua nafasi ya Mhandisi Nyamuhanga ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

“Askari polisi waliendelea kuzunguka na watuhumiwa kwa kutumia magari na mafuta ya serikali, wakavuka Kigongo Ferry kuelekea Sengerema. Niliwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ili wakamatwe… Iliwekwa road block na wakamatwa. Askari wale wakaanza kupiga king’ora eti walikuwa wanawafukuza kumbe walikuwa wanawasindikiza.

Rais Magufuli akimuapisha Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.Kabla ya Uapisho huo Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Athumani Diwani Msuya ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

 

“Nakupongeza tena IGP kwa kuwashughulikia askari hao, tena huyo Superintendent wa Polisi aliyekuwa akisindikiza huo mzigo umemvua cheo, na watapelekwa kwenye mahakama za kijeshi kisha mahakama za kiraia,” alisema Magufuli.

 

Aidha ameitaka Wizara ya Madini na Tume ya Madini kufanya kazi kwa weledi na kwamba watendaji wabuni kitu kitakachokuwa na maslahi ya Watanzania.

Loading...

Toa comment