JPM AFANYA UTEUZI CHUO KIKUU MUHIMBILI

Rais  John Magufuli amemteua Prof Andrew Barnabas Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa Prof. Pembe umeanza siku ya leo.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Pembe alikuwa Mhadhiri  na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri.
Loading...

Toa comment