JPM Amjulia Hali Askofu Ruwa’ichi Aliyelazwa MOI – Video

Rais Magufuli akiwa na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakimuombea Askofu Ruwa’ichi.

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi ya MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa jana usiku.

Rais Magufuli akiwa na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakimuombea Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya MOI.

Askofu Ruwa’ichi anapatiwa matibabu katika Taasisi ya MOI baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa juzi, Jumatatu, Septemba 9, 2019 usiku.


Loading...

Toa comment