The House of Favourite Newspapers

JPM Ampa Mtoto Mlemavu Milioni 5, Hatembei Wala Kukaa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa msaada wa Tsh. Milioni tano baada ya kuguswa na hali ya mtoto mlemavu, Latifa Ibrahimu ambaye hawezi kutembea wala kukaa.

Akikabidhi msaada huo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 kwa familia ya Bi Rehema Kadogosa ambaye ni mama mzazi wa mtoto Latifa, mkazi wa Mwenge Mlalakuwa jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Rais Magufuli, gusa Dismas Samike kuwa Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu (Comptroller State House – CSH), amesema Rais ametoa msaada huo baada ya kuguswa na hali ya mtoto huku akiwataka akina baba kutokimbia majukumu yao anapozaliwa mtoto mwenye ulemavu ndani ya familia zao.

 

Mama mzazi wa Latifa, Bi Rehema baada ya kupokea msaada huo, amemshukuru Rais Magufuli kwa namna anavyowasaidia Watanzania hasa wananchi wanyonge ambao hawajiwezi.

 

Kwa yeyote mwenye ataguswa kutoa msaada zaidi kwa mtoto Latifa, anaweza kuwasiliana na mzazi wa mtoto huyo kupitia namba za simu 0713 323 305 au kuwasilisha mchango wake kupitia akaunti namba 015 233 775 9200 kupitia Benki ya CRDB tawi la Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.