RAIS John Magufuli leo Januari 31 Januari, 2020, amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Susan Mlawi. Kabla ya Uteuzi huo, Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Pia amemteua Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Suleiman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali Mpya wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.





