JPM Atua Namibia, Apokelewa na Rais Hage – Pichaz

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  John Magufuli amewasili nchini Namibia leo Jumatatu, Mei 27, 2019, na kupokewa na mwenyeji wake Rais, Hage Geingob wa Namibia katika kulu ya nchi hiyo, jijini Windhoek.

Magufuli amewasili nchini humo kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku mbili akitokea Pretoria nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa Rais  Cyril Ramaphosa.

Akiwa namibia, Magufuli anatarajiwa kufungua mtaa uliopewa jina la rais wa kwanza wa Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere unaoitwa Mtaa wa Mwl. Nyerere.


Loading...

Toa comment