JPM Awapa Fedha Majeruhi wa Morogoro, Kutibiwa na Serikali – Video
RAIS Magufuli leo Agosti 11, 2019 amewatembelea majeruhi 43 wa ajali ya moto iliyotokea jana mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuwapatia kila mmoja Sh500,000 kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Ajali hiyo ilitotokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika mtaa wa Itigi, Msamvu mkoani Morogoro mita 200 kabla ya kufika kituo cha mabasi cha Msamvu barabara ya Morogoro- Dar es Salaam baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.
Majeruhi 46 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro walihamishiwa MNH. Hata hivyo, watatu kati yao wamefariki dunia leo.
Akiwa katika wodi ya Sewahaji na Mwaisela, alizungumza na majeruhi hao kuwashukuru wauguzi pamoja na madaktari kwa huduma nzuri na kuwazawadia Sh1 milioni.
Comments are closed.