The House of Favourite Newspapers

JPM Awapa Viwanja Taifa Stars, Awataka Wajitume Zaidi – Video

RAIS . John Magufuli amewazawadia viwanja vya kujenga nyumba jijini Dodoma wachezaji wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, viongozi wao, bondia Hassan Mwakinyo na mwalimu wake kwa ushindi wa jana dhidi ya Uganda na kutinga kwenye fainali za mashindano ya ubingwa wa nchi za Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Misri mwaka huu.

Bondoa Hassan Mwakinyo amezawadiwa kutokana na ushindi alioupata dhidi ya bondia wa Argentina katika pambano lililofanyika nchini Kenya.

Magufuli ametoa zawadi hiyo leo Machi 25, 2019, Ikulu, jijini Dar es Salaam,  wakati alipokutana na wanamichezo hao ambapo pia alikula nao  chakula cha mchana.

“Niwapongeze Watanzania, hongereni sana, jana tulishuhudia uzalendo wa kweli, hapakuwa na mambo ya klabu, vyama, wala tofauti yoyote, uzalendo ule ulikuwa mkubwa mno, tukiuweka kwenye mambo mengine yote tutafika mbali sana.

 

“Mimi sina kitu cha kuwapa, lakini tamko langu kwa niaba ya Watanzania wote ninawapa zawadi ndogo nyinyi wachezaji wa Taifa Stars, viongozi wenu, Leodgar Tenga, Peter Tino, na Mwakinyo.  Tutawapatia viwanja vya kujenga nyumba,” alisema na kumwagiza  Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa)  kuhakikisha analifuatilia suala hilo.

 

 

Rais pia aliipongeza Kamati ya Ushindi iliyokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, vyombo vya habari na Watanzania wote kwa pamoja na kutoa Sh. bilioni moja kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo ya taifa.

 

Pia alimzawadia shilingi milioni tano mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Peter Tino, ambaye ndiye mfungaj wa bao lililoipeleka Tanzania AFCON mwaka 1980, ili akaongeze mtaji katika shughuli anayoifanya.

FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.