JPM Azuia Ushuru Machinjio Vingunguti, Amwagiza Makonda

RAISĀ  John Magufuli ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Ilala kutochangisha fedha katika machinjio ya Vingunguti hadi pale watakapokamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Rais Magufuli amesema hayo, alipofanya ziara ya kushtukiza na kuwataka viongozi wa halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wengine kuangalia namna ya kukamilisha kazi hiyo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Amesema, kuanzia sasa mkurugenzi wa halmashauri na watendaji wengine ni marufuku kukusanya ushuru wa aina yoyote sambamba na kuwataka kufanyia kazi maagizo yake usiku na mchana.

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa eneo hilo la machinjioni ambalo linadaiwa kukusanya takribani milioni 100 kwa mwezi.

Rais alipita hapo akitokea kwenye uzinduzi wa rada kwa ajili ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kiwanda cha mabomba ya plastiki kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Toa comment