The House of Favourite Newspapers

JPM: Hatujawahi Kupata Hata Senti Tano Kutoka Airtel – VIDEO

Kampuni ya Mawasiliano ya Bharti Airtel, leo Jumanne, Januari 15, 2018 imesaini mkataba na Serikali ya Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali katika Kampuni ya Airtel kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49.

 

“Airtel imeanzishwa zaidi ya miaka tisa iliyopita na katika kipindi hicho chote hatujawahi pata faida hata senti tano, kila siku ni hasara tulikuwa tunapata gawio zero japo tulikuwa na Hisa Asilimia 40 . Pamoja na kuwa tulikuwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 40, hatukuwahi kupata gawio lolote kutoka Bharti Airtel, hii inadhihirisha kulikuwa na uwekezaji wa ufilisi.

 

Wamesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano watakuwa wanatoa Bilioni 1 kila mwezi katika kipindi cha miaka mitano lakini Chairman mwenyewe amesema atatoa US Dollar Milioni 1 ipelekwe kwenye miradi ya kijamii,

 

Huu ni ushindi kwa Taifa letu, ni ushindi mkubwa kwa Airtel na kwa uwekezaji, Mtu mwingine angesema Tanzania haihitaji uwekezaji lakini tunataka wawekezaji na ndio maana tuna kituo cha uwekezaji (TIC). Tanzania iko vizuri na watu wake ni wapole,” alisema Magufuli.

 

Awali, Waziri wa Katiba na Sheria imesema Mazungumzo kati ya Serikali na Bharti Airtel yamechukua miezi 8 na Serikali imefanikiwa kuongeza hisa kutoka 40% hadi 49% bila kulipia chochote.

 

“Katika Menejimenti ya Airtel tumekubaliana katika nafasi kuu tatu ya Chief Executive Officer, Chief Technical Officer na Chief Finance Officer, nafasi moja itapewa Watanzania yaani Serikali ya Tanzania itateua Afisa Mkuu Ufundi na Bharti Airtel itamuajiri,” amesema Waziri Kabudi.

Comments are closed.