JPM: “HIYO SADAKA NILIYOIKUSANYA MKAIHESABU VIZURI, NILITAMANI NIWE PADRI” – VIDEO
Rais Magufuli leo ametoa hotuba katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu Mteule, Gervas Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza Jimbo Kuu Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya, ambapo amepongeza askofu huyo kwa kuteuliwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo hilo.
Pia alisema yeye alipokuwa mdogo alitamani sana kuwa Padri ila hajui nini kilimtokea mpaka akashindwa hata kuwa Katekista wala Mwenyekiti wa Jumuiya, na inaonyesha wazi hii kazi ngumu.
Pia alimaliza kwa kibwagizo cha kusema sadaka aliyoikusanya yeye ikahesabiwe vizuri na hivyo kuamsha vicheko kwa waumini waliohudhuria ibada hiyo.


Comments are closed.