JPM, JK WAPAA SAUZI KWENYE SHEREHE – (PICHA + VIDEO)

Rais  John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Afrika Kusini asubuhi hii ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo,Cyril Ramaphosa, mjini Pretoria.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  John  Magufuli,  leo Ijumaa, Mei 24, 2019 amkwenda Afrika Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

…Akisalimiana na Rais Mstaafu, Jakaya  Kikwete,  kabla ya kuanza safari hiyo.  Katikati yao ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula.

Katika safari hiyo Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya  Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

…Akiongoza na Kikwete na Mangula (wa pili kushoto) kuelekea kwenye ndege.

Wakizungumza kabla ya kuondoka, Kikwete na Mangula wamesema Tanzania na Afrika Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba serikali na chama vina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.

Viongozi hao wametumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Magufuli na Kikwete wakipanda ndege.

Aidha, Prof. Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Ramaphosa, Rais Magufuli atafanya ziara ya kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua mchango wake kusaidia nchi za Afrika kupata uhuru.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Loading...

Toa comment