The House of Favourite Newspapers

JPM, Mama Janeth Wampa Wastara Mil 15/= Za Matibabu (Video)

Ngusa Samike ambaye ni Katibu wa Rais akiwasilisha mchango wa Sh. milioni 15 kwa mwigizaji Wastara  Juma kutoka kwa Rais John  Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu.
Samike (wa pili kulia) akiwa na watangazaji wa kipindi cha SHILAWADU baada ya kumkabidhi Wastara fedha hiyo.
…Akiongea katika hafla hiyo.

RAIS John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamechangia Sh. milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya msanii Wastara Juma ambazo ziliwazilishwa na Katibu wa Rais, Ngusa Samike nyumbani kwa msanii huyo. Pia aliwasilisha mchango wa Sh. milioni  moja na laki tisa kutoka kwa wasaidizi wa Rais.

 

Global TV ilikuwa ya kwanza kufika nyumbani kwa Wastara  na kufanya mahojiano naye ambapo alieleza kwa kina kilichokuwa kinamsumbua na pia alipata fursa ya kuwaomba Watanzania wamchangie ili aweze kupata matibabu ya mguu wake ambao ulikatwa miaka kadhaa kutokana na ajali ya barabarani.

 

Mahojiano hayo ya katika video ambayo imewekwa  chini, baada ya habari hii.

Baada ya hapo, magazeti pendwa ya Global Publishers  yaliandika habari hiyo yakiwaomba  Watanzania  kumchangia msanii na ndipo vyombo vingine vya habari nchini wakiwemo watangazaji wa wa kipindi cha SHILAWADU wakaiendeleza kampeni hiyo ambapo leo Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth wamemchangia msanii huyo.

 

Global Publishers na vyombo vyake wanatoa rai kwa Watanzania waendelee kumchangia msanii huyo ili aweze kupata matibabu yanayotakiwa.

PICHA/HABARI NA HILALY DAUDI/GPL

MASKINI WASTARA! Tazama Mguu Wake Ulivyoharibika, Anaomba Msaada

Comments are closed.