JPM: Museveni Fukuza Watendaji Wanaokukwamisha – Video

Rais John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, wamefanya kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kongamano hilo, Rais Magufuli amemtaka kuwa mkali kwa wanaokwamisha ujenzi wa bomba la mafuta huku akitolea mfano alipoingia madarakani alibadili Makamishna Wakuu wa TRA watano ili kuongeza ufanisi

“Nitumie fursa hii kutoa shukrani kwa Rais Museveni, mikutano kama hii inatoa fursa kwa wafanyabiashara wetu siyo tu kufanya biashara lakini pia kushughulikia changamoto zinazowakabili, ushirikiano kati ya Uganda na Tanzania na mafungamano yamekuwapo tangu enzi na enzi hata kabla ya ukoloni kiuhalisia sisi ni ndugu moja hata lugha na tamaduni zetu zinaonyesha hivyo,”

 

“Kwa bahati mbaya walikuja watu wakaweka mipaka wakatutenganisha lakini kwa namna yoyote ile mipaka hii haiwezi kututenganisha au kuondoa undugu wetu, tutaendelea kuwa kitu kimoja na kushirikiana.

 

“Mahusiano yetu yaliimarishwa zaidi baada ya kurejea kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyovunjika mwaka 1977, zikiwa miongoni mwa jumuiya mpya nchi zetu zimekuwa na dhamira ya dhati kuwa na ushirikiano wa kikanda.

 

“Mataifa yetu yanayo rasilimali za kutosha kabisa kuleta maendeleo hususani watu wetu na maliasili zetu, tunazo fursa za kukuza uchumi ikiwamo utalii, gesi madini, bidhaa za viwandani, kilimo, mifugo, uvuvi na mafuta.

 

“Tanzania na Uganda, zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika maeneo ya kilimo, uhamiaji, magereza na hati makubaliano ya kikao cha tatu cha tume ya pamoja ya kudumu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

 

“Swali la kujiuliza ni kwanini kiwango cha biashara na uwekezaji kimeendelea kuwa chini, kwa mfano nimetaja makampuni yaliyosajiliwa hapa ni 22 wakati Kenya ni 504, kwanini kiwango cha biashara Tanzania na Uganda kiko chini.

 

“Mimi tangu nimeingia madarakani nimebadilisha Makamishna Wakuu wa TRA mara tano. Sio jambo la kujivunia, ila inabidi. Sasa Mzee Museveni (sikufundishi), ila yule wako umemng’ang’ania siku zote, wa nini? Wanazichelewesha nchi zetu kupata faida,” amesema Magufuli.


Loading...

Toa comment