JPM: Natamani Niwe na MABILIONEA 100 – Video

RAIS John Magufuli leo amesema anatamani wakati akimaliza utawala wake na kuondoka madarakani, Tanzania iwe imeshatengeneza wafanyabiashara wazawa mabilionea zaidi ya 100 ili kuinua sekta ya biashara na uchumi nchini.

 

Magufuli amesema hayo leo Juni 7 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa 1,000 Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kuwa changamoto za ukwamishaji wa biashara kwa upande wa serikali ni kutokana na utitiri wa taasisi za udhibiti, rushwa, tozo na kodi mbalimbali zinazowakera wafanyabiashara hao.

 

“Kodi zikiwa chache na viwango vikiwa vidogo biashara inastawi, kinyume chake biashara hudumaa, hii ndiyo sababu tumeanza kuchukua hatua za kupunguza viwango na utitiri wa kodi.

 

“Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, miradi mipya iliyosajiliwa katika kituo cha uwekezaji ni 897 ambapo miradi 313 ni ya Watanzania, 377 ni ya wageni na 207 ni ya ubia kati ya Watanzania na wageni. Mimi ningependa nitakapomaliza muda wangu angalau niwe na mabillionea wafanyabiashara wa Tanzania zaidi ya 100, nitafurahi sana,” amesema.

TAZAMA VIDEO HAPA

Loading...

Toa comment