JPM: Ndege Yetu Iliyoshikiliwa Canada Imeachiwa

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imakamatwa nchini Canada imeachiwa na wananchi watatangaziwa siku ya kuwasili ili waipokee jijini Mwanza.

 

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa amesema hayo wakati anafungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Inayofanyika Jijini Mwanza.

 

“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza,” amesema Rais Magufuli.

 


Toa comment