The House of Favourite Newspapers

JPM, Rais Lungu Wazindua Kituo cha Huduma Tanzania na Zambia – (Picha + Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

KITUO cha huduma za pamoja kati ya Tanzania na Zambia kilichopo mpakani Tunduma kwa Tanzania na Nakonde kwa Zambia, kimefunguliwa rasmi na Marais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia.

 

Baada ya kufungua kituo cha huduma kwa pamoja kati ya Tanzania na Zambia, Marais wa Tanzania
Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia kila mmoja ameingia kwenye chumba cha nchi yake ishara ya kuanza rasmi kwa matumizi ya kituo hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia

Rais Magufuli;

“Niipongeze Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini zaidi niwapongeze zaidi Mamlka ya Mapato (TRA)’ kwa mwaka huu wamevunja rekodi kwa ukusanyaji wa mapato. “Leo tumefungua kituo cha kihistoria cha kiuchumi na kimuungano kwa nchi zetu mbili za Tanzania na Zambia.

Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

“Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Zambia kurudisha reli ya Tazara na kama kuna watu wanakwamisha Mimi nitumbue huku na Rais Lungu atumbue huko kwake.

 

“Zambia inaongoza kwa kupitisha mizigo mingi kwenye bandari ya Dar ambapo mwaka 2018 asilimia 38 ya mizigo yote ilkuwa ya Zambia, Takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Zambia kimeongezeka kutoka Tsh 89.2b hadi Tsh 265.6b.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda mti pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia .

“Mipaka hii isitucheleweshe katika kuboresha mazingira yetu ya ufanyaji wa biashara ndoto maana unaona Serikali imeamua kutengeneza mfumo wa kupunguza vikwazo hivyo na naamini kituo hiki kitakuza biashara zetu.

 

“Raisi wa Zambia anaitwa Lungu na mimi naitwa Pombe, najua na mnajua vizuri vitu hivi vikichanganyikana vinakuwaje na ukipigwa na rungu lililochanganyikana na pombe jeraha lake haliponi.

 

“Mimi nimeshazoea kubomoa tangu nikiwa Waziri wa Ujenzi kam umejenga katikati ya mipaka ya nchi hizi mbili uanze kuondoka usisubiri kubomolewa maana muda ukifika utabomolewa haitajalisha upo CCM au Chadema maana Maendeleo hayana chama.

Wafanyakazi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania na Zambia wakiwa tayari kwa kutoa huduma katika eneo hilo la mpakani.

“Wito wangu kwa wananchi wa pande zote mbili (Tanzania na Zambia) tumieni fursa na miundombinu hii kufanya biashara kwa maendeleo yenu,fanyeni kazi halali kwa bidii hatutavumilia watakaofanya kazi zisizofaa kama wizi na unga.

Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019

“Watendaji wote wa vituo hivi acheni kuwabugudhi wafanyabiashara na wasafirsihaji msisabahishe urasimu wala kujenga mazingira ya rushwa waacheni wafanyabiashara watajirike hilo ndio lengo langu na la Lungu.

 

“Kuanzishwa kwa kituo hiki cha huduma za pamoja kati ya Tanzania na Zambia cha Tunduma na Konde, kinakwenda kurahisisha shughuli zote za maendeleo, na wananchi niwaombe mkatumie hii fursa kuongeza kipato chenu.

 

“Niwatake watendaji na maofisa wote mnaohudumu kwenye kituo hiki, iwe wa Tanzania au wa Zambia, acheni kuwabugudhi wafanyabiashara na wasafirishaji, msitengeneze urasimu au mazingira ya rushwa, hatutawaacha salama.

Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia wakiwa na wafadhili wa mradi wakipanda mti kama kumbukumbu baada ya kuzindua Kituo cha Mpakani cha Tunduma-Nakonde One-Stop Border Post upande wa Tanzania Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019

“Kwa mliojenga kwenye mpaka anzeni kubomoa, mimi nilishazoea kubomoa kwahiyo msisubiri mpaka mimi nianze, hili nalisema wazi kwenu.

 

Rais Lungu;

“Kituo hiki cha Tunduma Nakonde ni moja ya vituo vikubwa Afrika. Kina uwezo wa kupitisha zaidi ya magari 600 kwa siku lakini pia kitaongeza ushindani wa biashara kati ya nchi hizi na kupunguza siku za watu kukaa mpakani.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsihi Mkuu wa Wilaya ya Nakonde Bw. Alex Sinkala kusimama baada ya kumpigia magoti kumshukuru kwa masada wa shilingi milioni tano taslimu ili kusaidia ujenzi wa Shule ya Sekondary ya Nakonde wakati akihutubiua wananchi wa Zambia Katika mkutano wa hadhara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Mpakani cha Nakonde-Tunduma One-Stop Border Post upande wa Zambia Leo Jumamosi Oktoba 5, 2019

“Chama changu cha United Party for National Development Patriotic Front kinaungwa mkono na watu wenye vipato vidogo na naamini hata kwako Rais Magufuli na CCM ni hivyo, kwahiyo lazima tuwatumikie na kuwajali hawa.

 

“Kwa wale ambao mmevamia na kujenga maeneo ya mipaka hususani raia wa Zambia nawaomba muondoke mapema wenywe vinginevyo nitachukua hatua sitahiki na mimi huwa sijali hata kama kesho ni uchaguzi nasimamia ukweli.

 

“Serikali zetu mbili hazikuchukua hatua kwa wafanyabiashara wakubwa bali hadi wadogo, ni muhimu kwa sababu wengi wanategemea biashara ndogondogo, wafanyabiashara wakubwa wanakuja na kuondoka lakini wadogo wapo kwa ajili yetu wakati wote lazima tuwasaidie sana.

”Dawati la pamoja la taarifa litasaidia kutunza takwimu za wafanyabiasra wadogo wadogo na kutoa taarifa kuhusu namna ya kupitisha mizigo katika eneo hili, na mamlaka za pande zote mbili kuhakikisha wanawasaidia wafanyabiashara wanapohitaji kuvusha biashara zao.

 

“Historia ya Zambia na Tanzania haiishi katika ujenzi wa kituo hiki kilichosainiwa mwaka 2010, uhusiano wetu ni muda mrefu kabla ya Uhuru wa nchi zote hivyo mimi ni nani mpaka nizuie ushirikiano huu.

 

“Najua mwenzangu ni ‘Bulldozer’ lakini na mimi ni Mtendaji kwenye mambo yangu, kama hutaki karoti utapata fimbo, waulizeni wenzenu ambao walishachapwa huko nyuma, hivyo wale waliojenga katika mipaka waondoke ili wapate zawadi lakini wale watakaobisha watapata fimbo,” Rais Lungu.

 

Comments are closed.