JPM: Tshisekedi Naomba Ukashughulikie Shida za Watu wa DRC – Video

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Antoine Tshisekedi,   amemaliza ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini akiwa amebeba ujumbe kutoka kwa Rais John Magufuli akimuomba akashughulikie kikamilifu matatizo ya watu wa DRC.

Magufuli aliyasema hayo siku ya mwisho wa ziara ya Tshisekedi katika hafla ya kumuuaga.

“Tumebadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa kwani ni vizuri kutetea maslahi ya ukanda wetu pamoja na bara letu kijumla. Naomba ukashughulikie shida za watu wa DRC kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo kwa sababu nchi hiyo haikutakiwa uchumi wake kukua kwa asilimia nne (4%) tu,” amesema Magufuli.

Alisema pia wamekubaliana kuwa rais huyo aimarishe bandari upande wa DRC ili pasiwe na matatizo wakati wa kusafirisha bidhaa, jambo ambalo liunahusu pia ujenzi wa barabara mbalimbali nchini  na usafiri wa anga  kupitia mashirika  ya nchi hizo mbili.

 

“Kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wetu, tumeamua kuifufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya nchi zetu, kwani haijakutana tangu mwaka 2002. Tumekubaliana mamlaka zetu husika na wafanyabiashara kufanya vikao vya ujirani mwema kwa ajili ya maendeleo yetu,” alisisitiza.

 

 

 

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

 


Loading...

Toa comment