The House of Favourite Newspapers

JPM: Wizara ya Kazi Wanatueletea Wafanyakazi Vilaza – Video

RAIS John Magufuli amefunguka na kusema kuwa amebaini kuna matatizo ndani ya Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana kuhusu watu wanaoajiriwa kwenye sekta mbalimbali za serikali na kuahidi kuwa atayashughulikia kwani tayari ameshayaona na anayatafutia ufumbuzi.

 

Magufuli ameyasema hayo leo Alhamisi, Juni 21,2018 wakati akipokea hundi ya Tsh. Bilioni kama gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania{TTCL} na kuzindua upanuzi wa huduma za TTCL katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

“Wizara ya Kazi kuna matatizo matatizo huko, nimeshayaona, nimeanza kuyafuatilia, kuna wengine vilaza kabisa lakini wanaletwa huku kuja kufanya kazi, hili nitalishughulikia, nalichomekea tu ili wabunge walitazame.

 

Aidha, Rais amesema amefuhai leo kwani, Juni 2016 serikali iliamua kuirejesha TTCL serikalini baada ya kununua asilimia 39 ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na BHARTI Airtel kwa gharama ya Tsh. 14.9 Bilioni ambapo kuanzia mwaka 2001 TTCL haikutoa gawio lolote kwa serikali hata senti 5, lakini baada ya miaka miwili tu leo TTCL imetoa gawio la Tsh. 1.5 bilioni.

 

“Nashindwa kujua tulikuwa tunaibiwa, au hujuma, au utendaji ulikuwa mbaya? Si kila muwekezaji ni mbaya, wengine wanawekeza kwa faida zao, sasa TTCL mnaonyesha shirika hili linazidi kukua. Ukweli kabisa nikisikia siku moja mmezalisha zaidi japokuwa nilishasema hakuna kupandisha mishahara mwaka huu, lakini kwa nyinyi mnaozalisha zaidi hata mkipandishwa mishahara ni safi tu.

 

“Kupitia mfumo huu wa nitawasiliana na Wakuu wangu wa mikoa kote nchini, na Dkt. Shein naye ataitumia kuwasiliana na wakuu wake wa mikoa huko Zanzibar ili kupunguza safari za kila mara mikoani,” alisema Magufuli.

Rais Magufuli Akipokea Gawio la Serikali Kutoka TTCL

Comments are closed.