The House of Favourite Newspapers

JUISI HAIWEKWI ASALI

PAMBEEE shoga wanakwam­bia ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia ucheze na siku hizi mwanaume hasifiwi kuvaa bali pochi, upo nyonyo? Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema iliyoniwez­esha kuandaa hiki nili­choamua kuzungumza nawe kupitia safu yetu hii. Shoga nilishawahi kuja na mada ya kuimba ukiwa uwanjani, mwan­amke sharti ujue jinsi ya kulichezea gitaa kisawa­sawa, imba nyimbo zote za Mchiriku, Singeli, Bongo Fleva hadi mwe­nyewe atakusapoti na ndiyo raha ya shabiki.

Sasa leo acha niwape somo wale ambao wak­ipewa chakula haraka­haraka kesho yake kukimbilia kwa jirani na kumsimulia, utasikia; ‘leo baby wangu ame­nilisha vijiko vingi hadi nimechoka! Ni fundi wa kulisha kweli tena kwa mikono yote’ sasa shosti unamwambia ili iweje, ina hu? Umeshamuam­sha mwenzako, akaam­ka na kuhamasika sasa akimtamani na yeye akapewa hicho chakula na mumeo utamlaumu nani?

Wengine wanafika mbali na kusimulia udhaifu wa mumewe utasikia; ‘Yaani shoga, mume wangu hakuwa hivi, siku hizi anarudi amechoka kweli, ananipa kijiko kimoja tu anadai amechoka’ sawa amechoka, wa kukusaidia kujua kwa nini amechoka ni jirani kweli?

Shoga juisi haiwekwi asali, jifunze kutunza siri ya chakula chako na mumeo. Iwe anakulisha kwa mikono yote, iwe anashindwa kukulisha hiyo ni siri yako na yeye. Mashoga wengine wao wakikaa kama kusu­kana au gengeni ama kwenye makundi ya Mtandao wa WhatsApp stori zao kubwa ni kila mmoja kumuelezea mumewe utasikia; ‘Leo usiku sijalala, nime­muandalia vyakula vyote, kala akaniambia hajashiba, basi hilo sebene la uwanjani mbona kashiba mwe­nyewe!’ Huko kushiba vipi tena?

Wengine wakiachwa wanaanza kulaumu kumbe aliyesababisha kuachwa huko ni yeye mwenyewe. Jamani mwanamke sharti uwe msiri, iwe unafurahia chakula cha usiku ama la kausha! Hiyo ni siri yako, mshirikishe mumeo, mwambie una­vyofurahia na unavyo­chukia pale anapokuli­sha.

Bibi zetu ndiyo maana walikuwa wakidumu sana kwenye ndoa zao kwani walikuwa wasiri sana. Hata wanyimwe chakula miezi na miezi huwezi kusikia cha kwa jirani wala mjumbe na kipindi hicho hakuna cha WhatsApp wala Fa­cebook labda mkutane kisimani na huko una­hesabiwa saa tu uwe umerudi. Makoo yao yaliwekewa kitu cha mgando na midomo yao haikuwa ikikaa wazi muda wote, upo shoga!  Kwa leo niishie hapa, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!

Comments are closed.