The House of Favourite Newspapers

Jukwaa La Biashara La Tanzania Na India (TIBF) Kuimarisha Mahusiano Ya Kibiashara

0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Angelina Ngalula akiongea viongozi wa kibiashara, makampuni binafsi na wageni waalikwa katika mkutano maalum wa kumkaribisha Spika wa Lok Sabha kutoka India Mhe. Om Birla aliyenchini kwa ziara ya kuendeleza mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania and India. Tukio hilo lilifanyika Januari 19 jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam, 19 Januari 2023: Jukwaa la Biashara la Tanzania na India (TBIF) limedhamiria kukuza mahusiano ya kibishara baina ya nchi hizo mbili kwa kuchochea ushirikiano katika sekta za kilimo, afya, teknolojia na nishati.

Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) akitoa neno kwa viongozi wa kibiashara, makampuni binafsi na wageni waalikwa wakati wa mkutano maalum wa kumkaribisha Spika wa Bunge la Wananchi wa India (Lok Sabha) kutoka India Mhe. Om Birla aliye nchini kwa ziara ya kuendeleza mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania and India.

Katika kutekeleza hilo, TBIF kwa kushirikiana na wadau wa kibiashara nchini, Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), wamefanya kikao maalum cha kumkaribisha Spika wa Bunge la Wananchi wa India, Mhe. Om Birla, aliye nchini Tanzania kwa ziara maalum akiambatana na wajumbe wa bunge, katika kukuza mahusiano baina ya Tanzania na India.

Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akiongea na viongozi wa kibiashara, makampuni binafsi na wageni waalikwa katika mkutano maalum wa kumkaribisha Spika wa Bunge la Wananchi wa India (Lok Sabha) kutoka India Mhe. Om Birla (kushoto )aliye nchini kwa ziara ya kuendeleza mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania and India.

Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan, Mwenyekiti wa TPSF Angelina Ngalula, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko na viongozi wengine wa kibiashara, wawakilishi wa makampuni binafsi nchini walihudhuria kikao hicho.

Spika wa Bunge la Wananchi wa India (Lok Sabha) Mhe.Om Birla akifurahia kupokea zawadi ya picha ya kuchorwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Biashara la Tanzania na India (TIBF )Gagan Gupta katika kikao maalum cha kumkaribisha wakati wa ziara yake nchini ya kukuza mahusiano ya kibiashara aliyoambatana na wajumbe wa bunge. Pembeni kulia ni Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan. Hafla hiyo ilifanyika January 19 jijini Dar  es Salaam.        
Leave A Reply