Julio: Hakuna wa Kumnyima Namba Ajibu Simba SC

BAADA ya Ibrahimu Ajibu kusaini Simba, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jamhuri kihwelo ‘Julio’, amefunguka kuwa hakuna atakayemuweka benchi mchezaji huyo ndani ya Simba.

 

Julio kwa sasa amepumzika kufundisha soka baada ya kuachana na timu ya Dodoma FC iliyokuwa ikishiriki daraja la kwanza ambayo kwake ilikuwa ya mwisho kuifundisha.

 

Akizungumzana Championi Jumatatu, Julio alisema kuwa Ajibu amefanya uamuzi ambao kwake umekuwa ni sahihi, hivyo kutokana na kipaji alichobarikiwa na akijituma zaidi, basi hakuna atakayemuweka benchi Simba.

 

“Ajibu ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana hapa nchini na maamuzi aliyoyachukua kwenda Simba ni mazuri kwa mtazamo wake na kwa kuwa ana uwezo mkubwa na akiongeza juhudi basi hakuna atakayemuweka benchi katika kikosi cha Simba,” alisema Julio.

 

Ajibu Jumatano alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga ambako alicheza misimu miwili ya ligi kuu.

Loading...

Toa comment