The House of Favourite Newspapers

Julio: Simba Mpeni Muda Sven Mtafurahi

0

KOCHA wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kumpa muda kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck, kwani kocha huyo ana uwezo mkubwa wa kufundisha.

 

Julio aliongeza kuwa mashabiki wa Simba wanakosea kumzomea kocha huyo pale timu inapokosa matokeo mazuri kwa kuwa bado anapambana kuingiza mifumo yake katika timu hiyo ambayo aliikuta katikati ya mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2019/20.

Hivi karibuni mashabiki wa Simba, walimzomea kocha huyo baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania na wakitaka aondoke kwenye timu hiyo wakidai kuwa hana uwezo wa kuifikisha mbali timu yao, huku wengi wao wakitaka kocha huyo aondoke klabuni hapo.

 

Akizungumzana Championi Ijumaa, Julio alisema Sven hana alichofundisha kwa muda mfupi huu aliokaa klabuni hapo, hivyo wachezaji wanatumia uwezo wao binafsi ili kuipatia timu matokeo, hivyo Wanasimba wanatakiwa kuwa na uvumilivu na kumpa muda kocha huyo kwa kuwa bado anajaribu kuingiza falsafa zake.

 

“Mashabiki na wanachama wa Simba wanatakiwa kumpa muda kocha Sven, kwa sababu kwa muda aliokaa klabuni hapo ni ngumu wachezaji kushika falsafa yake, ni ngumu sana kocha mpya anapokwenda kwenye timu mpya, halafu mbinu zake zikakubali kwa haraka, hivyo apewe muda tu atafanya vizuri kwa kuwa anaonekana ni kocha mzuri,” alisema Julio.

Stori na Issa Liponda, Dar es Salaam

Leave A Reply